Song Information:
| Label: |
Song ISRC: |
| Copyright: |
Writers licence: |
Lyrics:
Times za mwisho ama kweli zimewasili, kila mmoja hapa nakwambia anastahili, kuisoma bibilia ifuatilie kamili, kuja kwa Yesu ama kweli kuna dalili, hebu jiulize kama we una ukweli ama kwako tu wajiuliza hili swali "are you a christian really?" ama tu ni siku za jumapili? Jambo la pili, Alikupa mwili na akili ili ujue tu ndiye anayestahili yule yule tu Mungu wa Izraeli, Mungu wa Yakobo, Danieli na Samweli anaweza kuwa mkarimu anaweza kuwa mkali kwa wale wanaojidai kwamba wao hawajali kuja adhibiwa usiseme ni ajali je hujui amekutengenezea mahali? Chorus: Ni Ngai Baba; aliwawacha watu wanyunyize damu ya Mwana vijana wazee wasipotee *2 Message ya msalaba, ni ujinga kwa wanaoangamia kwetu ni nguvu za kukimbilia muumba bingu na hata dunia, tulimkemea tukamsulubisha, kumbe ni kutuokoa, ugonjwa dhambi kutukomboa lakini bado hamjampokea anatwambia 'ni mimi tu naweza kusaidia nikufanye uwe kichwa tene usiwe mkia lakini nakwita kila saa hutaki kunisikia nabisha kila saa hutaki kunifungulia mkono wangu sio mfupi nishidwe kukuokoa maskio yangu sio nzito nishindwe kusikia, kwa kukosa hekima watu wangu huangamia Chorus: Ni Ngai Baba; aliwawacha watu wanyunyize damu ya Mwana vijana wazee wasipotee *2 Habari njema ona twawaletea ndio msije mkateketea ukiipuuza hautojitetea haukupata kuisikia upendo mkuu ni kule kufariki kwa ajili ya hawa marafiki tazama hivi ndivyo jinsi mumba alipenda watu kama sisi anajua kuwa unadhani hakupendi eti amekulaani umeshindwa wa kuokoa n'nani ni damu yake tu msalabani haijalishi una dhambi kiasi gani ama mzigo mzito toka zamani ukiamini mkaribishe ndani akupumzishe akuoshe yaani..
|